Bonanza hili litaambata na semina ya vijana pamoja na kufanya utalii wa ndani katika maeneo ya kihistoria ya kaole ruins.
Ili kushiriki, kila kijana anahitajika kuchangia Tsh Elfu Ishirini na tano tu (TZS 25,000) ikiwa ni gharama za usafiri, chakula, kiingilio na vifaa vya michezo.
Kwa wale watakaopenda kupatiwa form ili kuweza kuchangisha fedha hizi wanaombwa wamuone Kiongozi yeyote wa umoja wa vijana au kumpigia simu mwenyekiti (elly- 0715 384 862).
Kwa wale ambao hawatahitaji form na wapo tayari kuchangia fedha hizo wao wenyewe, wamuone mtunza hazina wa umoja wa vijana au kiongozi yeyote na kumkabidhi fedha hizo. Hakikisha umeandikwa jina lako na kiasi ulichotoa.
Mwisho wa kukusanya michango itakua jumapili ya tarehe 15 feb 2015.
Mungu awabariki nyote.
