Wapendwa Wakristo
Nawasalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu kristo
Kwa niaba ya uongozi mzima wa umoja wa vijana wa kikristo usharika wa kurasini. Tunapenda kuwa takia heri ya christmas na sherehe njema za mwaka mpya.
Ni imani yetu kua yale yote mliomwomba Mungu awafanyie kwa mwaka huu wa 2014, amewajibu maombi yenu hasa hasa kwenye swala la afya njema na uhai hata kuweza kuiona siku hii nyingine ambayo sisi kama wakristo tunakumbuka kuzaliwa kwa bwana wetu Yesu krsito.
Pia ni imani yetu kua katika kipindi hiki cha sikukuu tutaenda kutenda yale yanayompendeza Mungu na hivyo kutojihusisha na anasa za aina yoyote.
Ni imani yetu kua tutaenda kuwa na sikukuu yenye baraka na Amani tukizidi kumtukuza Muumba wetu na kukumbuka kuzaliwa kwa bwana wetu Yesu kristo.
Bwana Awabariki sana
No comments:
Post a Comment